The House of Favourite Newspapers

Lwandamina Akosekana Leo, Kikosi Kamili Cha Yanga SC Vs Singida Hiki Hapa

Klabu ya Yanga imetangaza kikosi chake kitakachocheza dhidi Singida United Uwanja wa Taifa leo  bila kumtaja Kocha wao Mkuu, George Lwandamina kama ilivyozoeleka wakati wanapotoa majina ya wachezaji.

 

Jana taarifa zilianza kuzagaa kuwa kocha huyo raia wa Zambia ametimka kimyakimya bila kumuaga kiongozi yeyote wa timu hiyo na kuachana na Wanajangwani hao ambao alikuwa anamaliza nao mkataba mwishoni mwa mwezi ujao.

Chanzo cha ndani kutoka kwenye klabu ya Yanga kinasema kuwa meneja wa timu hiyo alikwenda kumpitia kocha huyu asubuhi ili aweze kwenda naye mazoezini lakini hakumkuta na hakupewa taarifa yoyote kuwa amekwenda wapi.

“Meneja mara zote ndiye amekuwa akimpitia na kwenda naye mazoezini, lakini alipofika asubuhi alikuta kwake kumefungwa na hakuna taarifa yoyote.

Lwandamina Atimka Yanga, Atua Zesco

 

Comments are closed.