The House of Favourite Newspapers

LYYN NA MOBETO IKO HIVI

MUUZA sura ambaye kwasasa ameamua kujitosa rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva Irene Godfrey ‘Lyyn’ amezungumzia ishu yake kwamba anashindana na mwanamitindo maarufu Bongo Hamisa Mobeto.

 

Lyyn ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa Chomeka siku tatu baada ya Hamisa kuachia audio ya wimbo wake unaoitwa Sawa.

 

“Watu wanapenda kuunganisha mambo sana sasa mimi na hamisa wapi na wapi, kwanza tunafanya muziki tofauti japo zote ni Bongo fl eva lakini hazifanani kama ukisikiliza kwa makini sasa nishindane nae ili iweje.

 

“Kwanza nilikua hata sijui kama katoa audio, msiunganishe mambo jamani mkagombanisha watu sio vizuri wote tunatafuta maisha,” alisema Lyyn.

Comments are closed.