The House of Favourite Newspapers

Lyyn: Sina tatizo na Tanasha

0

MREMBO anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Irene Godfrey ‘Lyyn’ amefunguka kuwa yupo tayari kufanya ngoma na mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’, Tanasha Donna.

Akizungumza na +255 Global Radio juzi baada ya kutembelea Global Group, Lyyn alisema haoni tatizo kufanya kolabo na Tanasha hata kama naye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond au Mondi.

“Sina tatizo na Tanasha ikitokea tutafanya tu kolabo, yeye ni msanii na mimi pia ni msanii kwa hiyo tunaweza kufanya tu hiyo haina shida,” alisema Lyyn.

Lyyn alizidi kutiririka kuwa aliachana na Mondi kitambo kabla hata hajaanza kufanya muziki na haoni tatizo kushirikiana na mrembo huyo ambaye anammiliki Mondi kwa sasa. Ili kupata mahojiano kamili, ingia YouTube, tafuta Global TV.

Leave A Reply