The House of Favourite Newspapers

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani Yafanyika Hifadhi ya Serengeti

0

Taasisi ya Doris Mollel Foundation imeadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo kwa kawaida huadhimishwa mnamo tarehe 17 Novemba kila mwaka, kwao maadhimisho hayo yamefikia kilele jana, Novemba 20, 2022 ambayo ni Siku ya Mtoto Duniani na yanafanyika katika viwanja vya Robanda, vilivyopo katika Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara.

 

Wadau mbalimbali wa maendeleo walioungana na Doris Mollel Foundation kupanda balloon na kutalii katika Hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kukuza utalii na kuhamasisha kujitolea, na pia wanatarajia kupandisha ujumbe wa Watoto njiti katika kilele cha Mlima Kilimanjaro baada ya tukio la jana.

 

 

Licha ya kufanya Utalii Serengefi, Doris Mollel Foundation, wamejipanga na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zitaambatana na kukabidhi misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo nchini, ambao ni; TIKA, Aga Khan Hospital, Oryx Energies Tanzania na Freo2 Foundation

 

Wengine Miracle Experience, Coca Cola Tanzania, Precision Air Tanzania, Anudha Limited, Ashton Media, Nest360, na Ifakara Health Institute, ambao kimsingi, wanawashukuru sana kwa kuwaunga mkono katika kuhakikisha kuhakikisha maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti yanafana.

 

Katika maadhimisho hayo, Doris Mollel Foundation itakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 180,190,000 ambavyo vitakwenda katika hospitali za Wilaya za Serengeti, Ukerewe, Kwimba, na Magu, pamoja na ufungaji wa mitambo ya hewa oxygen kwa watoto wachanga katika hospitali za Siha, Karatu, Monduli na Dabaldi; pia itakabidhi mitungi 200 ya gesi yenye thamani ya shilingi 8,200,000 kwa ajili ya akina mama wajawazito katika Wilaya ya Serengeti.

 

Leave A Reply