The House of Favourite Newspapers

Maalim: Hatutasusia Uchaguzi Mwaka Huu (Picha + Video)

0
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad,  akisani kitabu cha wageni katika ofisi ya Global Group iliyopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam akiwa na Meneja wa +255 Global radio, Borry Mbaraka (kushoto mwenye miwani) na Mhariri wa Mwandamizi, Elvan Stambuli (katikati).

MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamadi amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ACT Wazalendo hakitasusia uchaguzi huo.

…Akinawa sabuni maalum kujikinga na Corona baada ya kuweka saini kwenye kitabu cha wageni.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wahariri wa Kampuni ya Global Publishers baada ya kufanya ziara katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

…Akipanda ngazi kwenye ofisi ya Global Group.

Alisema kabla ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kukubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF, Maalim pamoja na wafuasi wake walikuwa wameshafanya utafiti na kufahamu hatima yao kisiasa.

 

“Tuliunda kamati tukawaambia wapitie katika vyama washiriki wa Ukawa ili kuwauliza endapo watatupokea, na vyama vyote vilisema vitatupokea, ila waliokuwa wepesi zaidi ni ACT wazalendo ndio maana mahakama ilipoamua saa sita mchana sisi saa nane tunatangaza kwenda huko yaani ‘shusha tanga pandisha tanga’,” alisema.

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kulia) akiongea jambo na Maalim Seif.

“Kwa mfano wapo wanaosema tulivamia na kuchukua ofisi za matawi wakati si kweli, ni kwamba CUF ilikuwa na majengo mawili inayoyamiliki Mtendeni na Kilimahewa, mengine yote ni nyumba za watu binafsi ambao wao walitupatia nyumba zao kwa imani yao kwa CUF baada ya kuondoka wakabadili misimamo, kwamba ulipo Maalim na sisi tupo.

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Richard Manyota (kushoto) akiongea jambo na Maalim Seif akiwa na Elvan Stambuli (kulia), Bori Mbaraka (wa pili kutoka kulia) na nyuma ni Mhariri wa Global Digital, Walusanga Ndaki.

“Kwa hiyo hatujaenda huko kwa bahati mbaya, ukishajiunga  kwenye chama hiki baada ya wiki moja unaweza kugombea nafasi yoyote, na tumeendana vizuri kabisa kwa sababu nimeshinda kwa asilimia 97 ya kura. Ado Shaibu ambaye katibu mkuu kijana kabisa kapata asilimia 100 ya kura zake. Kwa hiyo uongozi ni mchanganyiko wa zamani na wapya,” alisema.

 

Mhariri wa Gazeti la Risasi, Erick Evarist (kushoto) akimkabidhi Gazeti la Risasa Mchanganyiko Maalim Seif.

“Naamini tutashinda kwa sababu kabla ya sisi na wenzangu kutoka CUF,  ACT Wazalendo ilikuwa na matawi machache sana lakini sasa hivi Zanzibar imebadilika na kuwa purple (zambarau), CUF ukitafuta hukioni tena,” alisema.

Muda wa mabadiliko ya tume bado upo

Aidha, alisema licha ya kwamba baadhi ya watu wanadai muda wa kuibadilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa tume huru hautoshi, si kweli kwa sababu muda upo wa kutosha.

“ Kinachotakiwa ni kupelekea muswada wa sheria bungeni kwa hati ya dharura, tena CCM wenye wabunge wengi wanaweza kupewa maelekezo tu kuupitisha muswada huo, kwa hiyo suala la muda kuwa mdogo hatukubaliani nalo.

Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Omary Mdose (kulia) akimkabidhi Gazeti la Championi Ijumaa Maalim Seif.

“ Ila hata kama hatukupata tume huru hatususii uchaguzi, sisi ni kujipanga tu kwenye uchaguzi huu.  Tumemaliza chaguzi zetu ndani ya chama kazi kubwa ni kushinda uchaguzi mkuu,” alisema.

 

Pamoja na mambo mengine alisema muungano wa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Ukawa mwaka 2015, bado upo.

Maalim Seif akiwa katika studio ya +255 Global Radio kabla ya kuanza kufanya mahojiano.

“Niseme kwamba kuna utashi kwenye vyama, kwamba tuzungumze ili tuweze kukubaliana tujifunze makosa ili yasijirudie tena,” alisema.

 

1

STORI: GABRIEL MUSHI, PICHA: MUSA MATEJA

Leave A Reply