The House of Favourite Newspapers

Yanga Yagomea Mabadiliko ya Mechi Yao na Simba

0

Muda mfupi baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusogeza mbele mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni na kutakiwa kuanza saa 1 usiku, Klabu ya Yanga imegomea uamuzi huo.

 

Kupitia taarifa iliyotoa timu hiyo kwa umma imesema kuwa wao watapeleka timu uwanjani saa 11 jioni kama ilivyokuwa awali na kuitaka Bodi ya Ligi kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni ambazo zinawataka kubadili ratiba saa 24 kabla ya mchezo.

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.

 

TFF imesema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Leave A Reply