The House of Favourite Newspapers

Mabadiliko ya YANGA Yanaitaji Muda

0

YANGA inaonekana kufanya usajili wa kisasa zaidi kwa sasa. Yanga ndiyo timu ambayo imesajili wachezaji wengi zaidi kwenye dirisha dogo. Yanga imekuwa na timu mbili tofauti ndani ya miezi sita kwa kuwa ni mwezi Agosti tu ilifanya usajili mwingine wa wachezaji wengi. Kipindi cha mwezi Agosti, Yanga walifanya mabadiliko ya wachezaji wengi sana. Hali hiyo itawafanya Yanga watumie muda mwingi sana kusubiria mafanikio.

 

Kitendo cha kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Kagera ni picha halisi kuwa Yanga wanatakiwa kufahamu kuwa wanatakiwa kuwa watulivu kama wanataka mafanikio. Kama Yanga wanaamini kuwa kufanya usajili kila mara kunaweza kuwasaidia nafikiri siyo kweli.

Siyo ajabu kama utawaona Yanga wanafanya tena usajili wa wachezaji wengi halafu wakaamini kuwa wanaweza kuanza msimu mpya kwa nguvu. Ili Yanga wafanikiwe kwanza wanatakiwa kukubali kuwa wanatakiwa kuandaa timu yao kwa muda mrefu ili wachezaji wazoeane. Kilichotakiwa Yanga ni utulivu na kuacha timu izoeane kwa kuwa ndiyo sera ya mafanikio ya timu yoyote duniani.

 

Timu kama Liverpool ambayo leo inawania ubigwa wa England imejiandaa kwa zaidi ya miaka mitatu ikiwa na wachezaji wengi walewale. Na utaona kwa sasa wamezoeana na wanacheza soka ambalo linaonekana kuwa linamanufaa kwa siku chache zijazo.

 

Hii inaweza kuwa moja ya njia ambayo Yanga wanaweza kuitumia kupata mafanikio lakini kama wataamini kuwa kusajili kila mara ndiyo dawa basi watakuwa wamepotea.

 

Lakini pia presha ya kocha mpya ya kila mara inaweza kuwa sababu pia. Yanga wameshinda na kutoa sare wakiwa na Charles Mkwasa, nafikiri walitakiwa kubaki naye. Mwisho nizipongeze timu zote za ligi kuu ambazo zimezingatia

 

usajili wao bila kukiuka taratibu kwa namna moja ama nyingine. Dirisha hili dogo ambalo lilifungwa usiku wa kuamkia jana

Alhamisi tumeona limekwenda kwa kisasa zaidi, hakukuwa na malalamiko mengi tofauti na misimu iliyopita. Hivyo nizipongeze timu zote ambazo zilikuwa bize sokoni wakati wa usajili na kuhakikisha hakuna dhuluma ambayo inalalamikiwa, mambo yalienda kwenye mstari hivyo kitu kama hiki kikiendelea hivihivi itakuwa safi.

 

Japokuwa awali kulikuwa na malalamiko ya mapema kwa Polisi Tanzania dhidi ya Yanga ambayo ilisamjili mchezaji wao aliyekuwa kwa mkopo kutoka Azam FC, Ditram Nchimbi lakini utaona timu zote zilikaa pamoja na kumaliza tofauti na sasa kijana anacheza.

 

Hivi ndivyo soka linatakiwa kwenda, timu zinazoendeshwa kisasa kama kuna tatizo zinakaa chini ya kumalizana vyema kabisa na kuachana bila manung’uniko yoyote.

 

Usajili umefungwa nina imani kila mchezaji amefurahia pale alipo kwa sasa hivyo atajitoa kwa nguvu zake zote kuhakikisha anatoa msaada wake kwenye eneo lake jipya la kazi. Sasa wanaume twendeni tukaonyeshane kazi uwanjani.

 

Leave A Reply