The House of Favourite Newspapers

Maajabu: Mtoto Atapika Mawe, Familia Yapigwa na Vitu Visivyoonekana

0

FAMILIA ya Bi. Laurastika Kweka wa Kata ya Bondeni, Mtaa wa Kilimambogo, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, inaomba  msaada wa maombi ili kunusuru hali iliyopo kwa sasa ya nyumba ya familia kupigwa  mawe na vitu visivyoonekana.

 

“Tatizo hili lilianza mwaka jana (2019) mwezi Machi ambapo mjukuu wangu wa kiume aliye darasa la sita kwa sasa, alianza kutapika mawe mazima-mazima bila kuwa na maumivu yoyote ila anapata shida kuyatapika.

 

“Nilimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Hai wakasema haumwi na palpale akatapika mawe.  Tulirudi nyumbani tukaenda kwenye maombi na hali hiyo iliisha kabisa, sasa juzi vitimbi vimeanza tena nyumba inarushiwa mawe mengi sana na tunakosa utulivu,” alisema.

 

Mashuhuda wa tukio hilo wamejionea mawe yakirushwa huku watu wakikimbia lakini mawe hayo haya hayampigi mtu badala yake yanadondokea pembeni kwa kishindo kikubwa japo ni mawe madogo.

 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Bondeni, Fahad Lema, aliyefika katika eneo hilo baada ya kusikia mkasa huo na mwanzo akisema  hauamini, alisema kweli aliposhuhudia mawe hayo.

 

“Hali hii inaogopesha sana, kwa kweli hii familia inateseka sana kwani wanashindwa kushiriki shughuli za maendeleo, muda mwingi wanapambana na hali hii,  jambo ambalo litazorotesha uchumi wa familia, hivyo kunahitajika utafiti pamoja na viongozi wa dini kusaidia familia hii,” alisema Lema.

 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kilimambogo, Fadhili Mwaha,  amekiri kuwepo kwa mkasa huo na kuomba watu wenye uwezo wa kutuliza au kuondoa kabisa tatizo hilo ili iweze kustawi na kwamba kitongoji kipo tayari kutoa ushirikiano kwa watakaofika kutoa huduma.

Huyu Ndiye Mwanafunzi Anaemuelewa Zaidi MAGUFULI ”Nikama Upepo”

Leave A Reply