The House of Favourite Newspapers

Madaktari 200 wa Cuba Watua Sauz Kupambana na Corona

0

Timu ya madaktari zaidi ya 200 wa Cuba imewasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi vya virusi vya corona. Afrika Kusini inaingia kwenye orodha ya nchi ambazo zitanufaika na juhudi za Cuba katika vita dhidi ya COVID-19 duniani.

 

Madaktari hao ni miongoni mwa wafanyakazi 1,200 wa huduma za tiba waliotumwa katika nchi 22 duniani ambazo zimeomba msaada wa nchi hiyo ya kikomunisti kuupiga vita ugonjwa huo.

 

Afrika Kusini itatarajiwa kuondoa marufuku wa watu kukaa ndani mwezi ujao.

 

Zaidi ya watu milioni 1.5 wataruhusiwa kurejea makazini na shule kadhaa ambapo pia ugawaji wa vyakula vilivyopikwa tayari na sigara vitaanza kuuzwa.

 

Lakini uuzaji wa vileo na mikusanyiko bado vitaendelea kupigwa marufuku.

 

Kuna wakati nchi hiyo kuna wakati ilikabiliwa na shambulio kubwa la maambukizi hayo, lakini wachunguzi wameshangaa jinsi ambavyo imepunguza kasi ya kuenea kwake.

 

Nchi hiyo imeripoti visa 4,361 vya watu waliokumbwa na virusi hivyo ambapo 86 wamefariki.

 

Baadhi ya wafanyakazi wa huduma za tiba nchini Cuba ambao wamesambaa katika nchi 22 duniani.

Leave A Reply