The House of Favourite Newspapers

Madaktari Bingwa India kutoa huduma Tanzania

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh akizungumza na wanahabari.
Daktari Bingwa wa Mifupa na Majeruhi katika Hospitali ya Aga Khan, Julius Dinda akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Prince Aly Khan Sanjay Oak(Kushoto) akizungumza

MADAKTARI  Bingwa kutoka Hospitali ya Prince Aly Khan ya Nchini India kwa kushirikiana na Madaktari wa Aga Khan wameanza kufanya upasuaji wa mifupa ya wagonjwa wa nyonga na magoti.

Akizungumza na wanahabari leo Mei 5, 2017 wakati wa utambulisho wa madaktari watatu kutoka Hospitali ya Prince Aly Khan ya jijini Mumbai nchini India, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh amesema wamekuja kwa ziara ya siku tatu nchini.

Akielezea ujio wao madaktari hao Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Lucy Hwai amesema madaktari hao watashirikiana na madaktari wa hospitali hiyo kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa mifupa na kutoa elimu zaidi kwa madaktari hao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh amesema hospitali yao imepanga kuboresha huduma zake kwa kufanya mradi wa upanuzi wa hospitali unaotarajiwa kukamilika Juni, mwaka huu kwa kujenga majengo ya wodi.

Amesema ujio wa madaktari hao bingwa utakua endelevu na kwamba utasaidia kuongeza ujuzi wa madaktari wa hospitali hiyo na wagonjwa watapata huduma ya upasuaji pasipo kusafiri nje ya nchi ambapo wataokoa gharama zikiwemo za usafiri.

Naye Daktari Bingwa wa Mifupa na Majeruhi katika Hospitali ya Aga Khan, Harry Matoyo amesema ujio wa madaktari bingwa hao ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya hospitali shiriki na Aga Khan ambao watashirikiana nao kufanya upasuaji wa mifupa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwa pamoja na matumizi ya kompyuta.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Prince Aly Khan, Sanjay Oak amesema lengo la ujio wao hapa nchini ni kuwawezesha madaktari kupata ujuzi ili kusaidia wananchi kupata huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu na kuokoa gharama za kusafiri nje ya nchi kutibiwa.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply