The House of Favourite Newspapers

Madaktari: Msitishwe, Fanyeni Haya Mkiambukizwa Msife

0

WAKATI nchi 163 duniani zikihaha kudhibiti kuenea kwa virusi ya Corona (COVID-19), madakari Bongo wamewatoa hofu wananchi kwa kusema wasitishwe zaidi na ugongwa huo.

 

Sambamba na kauli za madaktari hao ambao ni Dk. Isack Maro, Dk. Sizya Sadick na Dk. Dodfrey Chale wa jijini Dar es Salaam na uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko umeibuka na ripoti maalumu kuhusu namna virusi hivyo vinavyoua pamoja na mambo muhimu ya kufanya mtu anapoambukizwa ili virusi hivyo visiweze kumuua.

 

Ugonjwa huo ambao tayari juzi umebisha hodi nchini Tanzania kwa mgonjwa wa kwanza kudhibitika mjini Arusha, tayari umeathiri watu 190,356 duniani na kusababisha vifo 7,525 huku watu 80,886 wakipona.

 

NAMNA CORONA INAVYOUA

Kwa mujibu wa Mkurugezi wa Taasisi ya Tanzania Memorial Hospital, Dk. Maro, virusi vya Corona vinaingia katika mwili wa binadamu kwa kupitia njia ya hewa.

Dk. Maro alisema virusi hivyo vikishaingia huenda kuathiri sehemu ya juu ya mfumo wa hewa kwenye mapafu.

“Hapo ndipo mtu anapata mafua makali yanayoambatana na kichwa kuuma na mwili kuchoka.

 

“Hali hiyo ikiendelea bila kudhibitiwa ndipo husababisha homa ya mapafu ambayo ni -pneumonia, kwa sababu ina homa ya mapafu ina athari nyingi kubwa katika mwili wa binadamu na iwapo ikitokea kwa watu ambao kinga zao zimeshuka inasababisha mtu kupoteza uhai mara moja,” alisema.

 

Alisema Corona ambayo hugeuka na kusababisha mtu kupatwa na homa ya mapafu, husababisha mtu kushindwa kupumua kwa sababu kuta za ndani za vifuko vya kwenye mapafu huvimba.

 

“Vifuko hivi vikivimba huwa ni ngumu hewa kupita, yaani vifuko hivi hutumika katika mfumo wa ku-exchange hewa, hewa safi inatoka nje kuelekea kwenye damu, na hewa chafu inatoka ndani kuelekea nje.

“Sasa vifuko hivi vyembamba sana, kwa hiyo mwenye homa ya mapafu kuta hizo huvimba ndiyo maana mtu anashindwa kupumua, ndipo athari zinatokea na kusababisha kifo,” alisema.

 

MAMBO YA KUFANYA CORONA ISIKUUE

Kwa upande wake Dk. Chale alisema kuwa ugonjwa huo si tishio sana kwa uhai wa binadamu kwa sababu si wengi wanaokufa baada ya kuambukizwa.

Alisema mtu anapopatwa na Corona na kuthibitishwa kitabibu zipo njia za kufanya ili mtu huyo asiweze kupoteza maisha.

“Katika hali ya kawaida kinachoua siyo virusi vya Corona ni matatizo yatakayojitokeza kwa mtu mwenye virusi hivyo.

 

“Ukipata tatizo la kupumua hilo ndilo litakalokusababisha ufe lakini tatizo hilo lisipojitokeza au kesi nyingine za kiafya unaweza kuishi na wadudu hao hadi wakafa wenyewe kama yalivyo mafua, kwamba mtu anaweza kupata lakini baada ya muda yakatoweka hata bila kumeza dawa yoyote,”alisema Dk. Chale.

 

Aliongeza kuwa kitu muhimu zaidi katika kuhakikisha kuwa virusi vya Corona vinakosa nguvu ya kudhuru mwili hadi kuupelekea kupata magonjwa ni mtu kuhakikisha kuwa mwili wake unakuwa na kinga ya kutosha.

 

Hivi karibuni Wanasayansi nchini Australia wamesema kuwa wamegundua namna gani mfumo wa kinga mwilini unavyoweza kuupambana na virusi vya Covid-19 na kuvishinda.

Profesa Katherine Kedzierska ambaye ni miongoni mwa wanasayansi hao alinukuliwa na Jarida la Nature wiki iliyopita kuwa, kujenga mfumo imara wa kinga kunatosha kuwa kinga na tiba sahihi ya Corona.

 

Katika kulitolea ufafanuzi suala hilo Dk. Chale alisisiza kuwa kama yalivyo magonjwa mengine ndivyo ulivyo huu wa Corona kwamba unahitaji mtu mwenye kinga madhubuti mwilini kuweza kuushinda.

“Yako mambo mengi ya kufanya ili mtu aweze kuwa na mwili wenye kinga imara, kanuni za afya zimeeleza kwa kina lakini kichocheo kikuu cha uzalishaji wa kinga mwilini ni Vitamin C.

 

“Na vitamini hii hupatikana kwa wingi kwa mtu kula machungwa, matunda yote, mbogamboga, hapa namaanisha kuwa mtu akishaona amepata Corona anatakiwa kuzingatia ulaji bora.

“Kingine ambacho mtu hatakiwi kufanya anapougua Corona ni kuacha kunywa vinywaji vya baridi,” alisema Dk. Chale.

 

Aliongeza kuwa tabia ya virusi vya Covid-19 ni kupenda baridi hivyo mtu aliyeingiwa na vidudu hivyo akinywa vinywaji baridi anakuwa amepeleka kirutubisho kitakachovifanya virusi hivyo kukua hivyo daktari huyo akashauri watu kupendelea kunywa maji yenye vuguvugu yatakayosaidia kuviangamiza vidudu vilivyojificha kwenye koo.

 

TAKWIMU ZA VIFO VYA CORONA

Kwa nujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Diniani ‘WHO’, Tedros Adhanom Ghebreyesus idadi ya watu wanaopoteza maisha kwa Corona ni asilimia 3.4 kwa takwimu za Februari mwaka huu.

 

Ujumbe wa WHO uliotembelea nchini China ambako Corona ilianza kujitokeza uligundua visa vingi vya ugonjwa huo vilitolewa na watu wenye umri mkubwa huku vijana wakitajwa kuwa na uwezo wa kuishi na vijidudu hivyo bila kupata madhara jambo ambalo limethibitisha kuwa kinga za mwili ni muhimu katika kukabiliana na ugonjwa huo.

 

CORONA HUSHAMBULIA WATU HAWA

Uchunguzi kupitia mitandao mbalimbali umeonesha kuwa watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 60 kuendelea wana kinga ndogo ndivyo maana wamekuwa waathirika wakubwa wa virusi hivyo.

 

“Pia wale wenye maradhi kama kisukari, ukimwi, kansa yaani umepata ugonjwa ambao umeshusha kinga yako unapata ugonjwa huo kwa urahisi zaidi,” alisema Dk. Sizya alipofanya mahojiano na mwandishi wetu kuhusu ukweli wa watu wazima kuwa katika hatari ya kuambukizwa Corona kuliko vijana.

 

NCHI ZINAZOONGOZA KWA CORONA DUNIANI

Hadi sasa China ambako ugonjwa huo ulioanzia mapema mwaka huu, kuna visa 80,881 vimeripotiwa, kati yake vifo 3,226 na waliopona ni 68,715.

Italia ni nchi ya pili ambapo ina visa 27,980 vilivyoripotiwa, vifo 2,158 na waliopona ni 2,749.

 

Iran ni nchi ya tatu duniani ambapo kuna visa 16,169, vifo 988, na waliopona ni 5,389.

Aidha, hadi jana takwimu zinaonesha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki, Rwanda ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wagonjwa saba, Kenya saba na Tanzania sita.

 

TAHADHARI NI MUHIMU

Pamoja na madaktari kutoa taarifa za kuwepo vifo vya watu wachache vilivyosababishwa na virusi hivyo, bado ugonjwa huo ni hatari kwa binadamu hivyo hatua za kujikinga zinazotangazwa lazima zizingatiwe kwani wahenga walisema kinga ni bora kuliko tiba.

 

STORI: Waandishi Wetu, Risasi

Leave A Reply