The House of Favourite Newspapers

Madam Ruti aitwa Canada

0

Na Issa Mnally

MWIMBAJI anayefanya vizuri katika muziki wa Injili nchini, Madam Ruti ameitwa nchini Canada kushiriki katika tamasha la kimataifa litakalofanyika jijini Ottawa baadaye mwezi ujao.
Akizungumza na gazeti hili, Madam Ruti Mwamfupe alisema anajiandaa kwa ajili ya kulitendea haki tamasha hilo, hasa wakati huu akiwa ametoa albamu yake mpya ijulikanayo kama Kesho Yako Inakuja, yenye nyimbo sita.
“Nimepania sana mwaka huu niutendee haki muziki huu wa Injili, maana nyimbo zilizomo kwenye albamu hii zote zinamtukuza Mungu kwa nguvu zote ambazo ni Ebenezer, Utukufu ni Wako, Mungu Niumbie, Mkono wa Bwana, Kesho Yako Inakuja na Nasikia Kuitwa, albamu kwa sasa ipo madukani,” alisema.

Leave A Reply