testiingg
The House of Favourite Newspapers

Madereva 14 Watelekezwa Na Mwajiri Wao-Walala Nje Kwenye Miti, Waiomba Serikali Kuingilia Kati – Video

0


Madereva 14 wa magari ya masafa wanadai kutelekezwa kwa zaidi ya siku 7 katika mpaka wa tunduma na mwajiri wao baada ya kusafirisha Magari ya IT kutoka Dar es salaam na kwenda Nchini Zambia bila kupewa ujira kinyume na makubaliano na Mwajiri wao kampuni ya Thosma company limited kutoka Dar er salam.

Madereva hao wamefika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe ili kuomba msaada wa Serikali baada ya kutelekezwa mpakani hapo kwa muda wa siku saba huku wakikosa huduma ya Malazi na chakula.

Akizungumzia swala hilo Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Tanzani Bwana Schubat Mbakizao amekiri kuwapokea na kuwahifadhi kwa muda wakati wakifanya mawasiliano na mwajiri na kuamua kuwapeleka katika ofisi za mkuu wamkoa wa Songwe baada ya kukosa ushirikiano na kampuni hiyo.

Mwakilishi wa Kampuni ya Thosma mjini Tunduma bwana Fadhili Ngoya amesema kuwa Changamoto ya madereva hao imetokana na madereva hao kutokuwa waaminifu na kusababisha upotevu wa vipuli na kuisababishia hasara kampuni jambo ambalo linawalazimu kufika katika ofisi kuu ya kampuni kwaajili ya kutathmini Hasara iliyotokea.

Leave A Reply