The House of Favourite Newspapers

Madereva daladala wagoma Moro, abiria wakwama

1

moro (1)

moro (5)

Baadhi ya daladala zikiwa zimeegeshwa wakati mgomo ukiendelea.

moro (4)Wakati mgomo ukiendelea kamera yetu iliwanasa madereva na makondakta wakicheza soka katikati ya stendi ya mabasi na mpaka mpiga picha wetu anaondoka eneo hilo, timu ya madereva ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1.

moro (2)

Barabara za Manispaa ya Morogoro zikiwa tupu bila daladala wakati wa mgomo huo.

moro (3)

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akiongea na wanahabari.

Na Dustan Shekidele / GPL, Morogoro
WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro leo asubuhi wamekwama kwenda kwenye shughuli zao kufuatia daladala zote za manispaa hiyo kugoma kutoa huduma wakishinikiza kuachiwa kwa madereva wenzao walikomatwa na polisi.

Imeelezwa kuwa sababu za mgomo huo ni kupinga madereva wenzao kukamatwa na kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi kwa zaidi ya siku sita (6) sasa bila kupewa dhamana wala kufikishwa mahakamani.

“Dereva mwenzetu na kondakta wake wamekamtwa na leo ni siku ya sita, tukienda kuwawekea dhamana tunaambiwa tukae mita 100 mbele ya kituo cha polisi wakati familia za wenzetu hao zikiendelea kutaabika” alisema mmoja wa maderva hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Maga.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini dereva wa daladala hiyo inayofanya safari zake kati ya mjini kueleka Kijiji cha Mlali alikamatwa na polisi akiwa na madumu ya petroli kwenye gari lake huku akiwa na abiria jambo ambalo ni hatari kwa abiria hao.

Mtandao huu uliongea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, ambaye alikuwa na haya ya kueleza, “Muda huu nimetoka kwenye kikao na madereva wa daladala baada ya kikao hicho kilichohusisha pia viongozi wa SUMATRA, Mkurugenzi na viongozi kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya, madereva wamekubali kurejea kazini” alisema Kamanda Paulo.

1 Comment
  1. […] kazi ya ukondakta hapa nchini Tanzania inafanywa na wanaume lakini kutokana na ugumu wa maisha na kuongezeka kwa […]

Leave A Reply