The House of Favourite Newspapers

Madereva wa Daladala Mkoani Songwe Wagoma Kutoa Huduma ya Usafirishaji

0
Madereva wa Daladala mkoani Songwe

Madereva wa Daladala za Tunduma Mpemba Mkoani Songwe wamegoma kutoa huduma ya usafirishaji kwa madai ya Maslahi madogo. Wakizungumza na Global Tv madereva hao wamedai mupanda kwa mafuta kulikopelekea wao kupandisha nauli kutoka Tsh 500 Kila kituo mpaka Tsh 1000 bei ambayo haijaungwa mkono na serikali pamoja na wadau wa usafiri wa daladala hizo.

Mgomo huo umetokana na Serikali kufanya operesheni ya kuzuia upandishaji wa nauli kiholela.

Abiria wakiwa wanatahamaki baada ya kukosa huduma ya usafiri

Kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kumechangiwa na vita inayoendelea barani Ulaya kwa mataifa ya Urusi na Ukraine

Leave A Reply