The House of Favourite Newspapers

Madiwani Manispaa Ya Kinondoni, UWT Na Viongozi Wa CCM Walivyowatendea Wadi Za Wazazi

0
Diwani wa Viti Maalum, Grace Mkumbwa akizungumza na vyombo ya habari baada ya kutoa msaada huo.

Dar es Salaam 4 Machi 2024: Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani madiwani wa viti maalum wanawake kutoka Manispaa ya Kinondoni jijini Dar, viongozi wa UWT Chama cha Mapinduzi na viongozi wengine wa chama hicho, leo walitembelea vituo vya afya vya Kawe, Bunju na Kijitonyama na kugawa misaada mbalimbali kwenye wadi za wazazi.

Muuguzi Mwandamizi wa Kituo cha Afya cha Bunju, Esther Chacha akitoa shukrani zake wakati akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake Grace Mkumbwa amesema wao kama madiwani wa Manispaa ya Kinondoni pamoja na viongozi wa UWT na Chama cha Mapinduzi wameona ni busara kutumia wiki hii inayoelekea siku Wanawake Duniani kuwakumbuka kinamama hao waliokuwa kwenye kipindi cha uchungu wa kujifungua ambapo mara nyingi kumekuwa na changamoto ya uhitaji wa vifaa mbalimbali.

Diwani Esther Mkumbwa (kulia) akimpa sehemu ya misaada hiyo mmoja wa wanawake aliyefika Kituo cha Afya cha Bunju kwa ajili ya kujifungua.

Grace amesema baadhi ya vitu walivyopeleka ni pamoja na mabunda ya pamba, gloves na vinginevyo.

Madaktari na wauguzi kwenye vituo vilivyopata msaada huo walitoa shukrani za kwa misaada hiyo ya kibinaadamu na kuwaasa Wasamaria wema wengine nao kuiga mfano kama huo kwani kwenye uuguzi mara kadhaa huwaga zinatokea changamoto za upungufu wa vifaa mbalimbali kwa kinamama hao lakini msaada huo unakuwa ni muhimu sana.

Zoezi hilo lilifika mpaka Kituo cha Afya cha Kijitonyama.

Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo, Muuguzi Mwandamizi wa Kituom cha Afya cha Bunju, Esther Chacha aliwashukuru madiwani hao pamoja na viongozi wengine walioambatana nao kwa kutumia siku hii ya Wanawake duniani ambayo kilele chake ni tarehe 8 mwezi huu kuwakumbuka wanawake wenzao hao.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply