The House of Favourite Newspapers

Madiwani Watano CHADEMA Wajiuzulu, Watimkia CCM

0

MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za kujiuzulu za madiwani watano wa Chadema Jiji la Arusha.

 

Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho tawala nchini Tanzania.
Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane.

 

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala.

 

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 30, 2019, Dk Madeni amesema Jiji tayari limeanzia mchakato wa kuzifikisha barua hizo katika ngazi nyingine.
“Ni kweli madiwani hawa wamejiuzulu na barua ninazo,” amesema.

 

Madiwani waliojiuzulu ni George Nditika (Baraa), Veronica Hosea, Glory Kaaya, na Jeni Severe (wote Viti Maalum) na Godfrey Soilel (Simon).

 

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alipoulizwa kuhusu madiwani hao amesema alikuwa na taarifa zao kuwa watajiuzulu. Novemba 19, 2019, meya wa Chadema Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alijiuzulu na kuhamia CCM.

Leave A Reply