The House of Favourite Newspapers

Maelfu Waandamana Kumuunga Mkono Mugabe

0

460x

Na Leonard Msigwa/GPL

Maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe wameandamana kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Harare, kwa lengo la kumuunga mkono Rais Mugabe aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 36.

4432Maandamano hayo yamekuja siku chache baada ya mlolongo wa matukio ya wapinzani wa kiongozi huyo mwenye miaka 92 kumtaka aachie madaraka. Wakilalamikia kushuka kwa uchumi, rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu.

5555Mgomo kazini ulioitishwa kupitia mitandao ya kijamii na mchungaji Evan Mawarire, mapema mwezi huu umepata mwitikio mkubwa nchi nzima kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.

44445Rais Mugabe jana jumanne alimpinga mchungaji  Mawarire kwa uwazi mbele ya halaiki huku akimtaja jina lake na kumwambia yeye na wafuasi wake wanaweza kuhama nchini Zimbabwe endapo wanaona hawana furaha kuishi nchini humo.

555555Wafuasi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumuunga mkono kiongozi huyo wakiwa na mabango mbalimbali yenye picha zake.

 

Leave A Reply