The House of Favourite Newspapers

Mafurikio Hanang, Hali ni Tete!

0

KAYA 91 katika kijiji cha Bassotu wilayani Hanang mkoa wa Manyara zimezingirwa na maji hali iliyosababisha wayahame makazi yao baada ya Ziwa Bassotu kufurika.

 

Hali hiyo imelilazimu Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kuifunga kwa muda barabara kuu inayounganisha mawasiliano kati ya Bassotu-Katesh na Singida kwa ajili ya usalama wa watu  na vyombo  vya moto.

Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Basotu, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Manyara, Paul Kasabago, amewataka viongozi wa eneo hilo kuchukua tahadhari kwa kuwalinda watoto wanaokwenda shule hadi hali itakaporejea kawaida.

 

Baadhi ya wananchi waliozungumza na kituo hiki wamesema kwa sasa afya zao zipo hatarini kwa sababu wanatumia maji yaliyochanganyikana na maji taka baada ya vyoo kujaa maji.

Diwani wa kata ya Basotu, Samwel Qaoga, amesema hali kama hiyo haijawahi kutokea katika miaka ya karibuni na kwamba walishachukua tahadhari mapema.

 

Mtendaji wa kata hiyo, Elizabeth Issalo, amesema kutokana na hali hiyo mashamba yameharibiwa vibaya huku nauli zikiongezeka maradufu kutokana na mzunguko wa safari kuwa mrefu.

Miongoni mwa nyumba zilizokumbwa na athari hizo ni pamoja na ya Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) mkoa wa Manyara, Rose Kamili.

MAKONDA – “MSIKUBALI, Wanataka TUZAE Tu, Unatetea MWANAFUNZI Kubeba MIMBA”

Leave A Reply