The House of Favourite Newspapers

Mtoto Darasa la 3 Apewa Mimba na Dereva Bodaboda

0

MTOTO mwenye umri wa miaka 13 (jina lake limehifadhiwa) ambaye alikuwa akisoma katika Shule ya Msingi Msakila Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amekatishwa masomo yake akiwa darasa la tatu kwa kupewa ujauzito ambao sasa una miezi saba na mtu aliyefahamika kwa jina la Salum Mayunga ambaye ni dereva bodaboda.

 

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, mtoto huyo amesema wazazi wake wote wawili walifariki na kuchukuliwa na ndugu ambao walimwambia aende akaishi na kijana huyo, bila kujali ni mwanafunzi na pia umri wake ni mdogo.

 

Consolata Mlaponi ni mmoja kati ya watu waliojitolea kumsaidia mtoto huyo ambapo amesema kuwa kwa sasa mtoto huyo anakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha, ikilinganishwa na umri wake ambao ni mdogo na hawezi kujitafutia chochote maishani.

 

Hayo yamefanyika wakati Jeshi la Polisi mkoani humo likianzisha oparesheni kabambe yenye lengo la kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Leave A Reply