The House of Favourite Newspapers

Mafuriko Jangwani: Mabasi ya Mwendokasi Yashindwa Kutembea – VIDEO

DAR: Abiria wa mabasi ya mwendokasi wamekosa huduma ya usafiri leo asubuhi, baada ya kampuni ya UDART kusitisha huduma hiyo kutokana na mafuriko eneo la Jangwani.


=======

TAARIFA KWA UMMA

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inaujulisha umma kuwa, huduma za mabasi hayo zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri tarehe 16/03/2018 kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Huduma zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Deus Bugaywa,

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART.

 

VIDEO: JPM Ammwagia Minoti Mama Ntilie Morogoro

Comments are closed.