The House of Favourite Newspapers

Mafuriko Yatokea Bukoba Mjini, Nyumba Zafunikwa

Baadhi ya nyumba zikiwa zimezungukwa na maji, mjini Bukoba

Mafuriko yameikumba Bukoba mjini leo kuanzia majira ya saa mbili asubui kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kufunika  na kuzunguka baadhi ya nyumba zilizopo maeneo ya Nyakanyasi na Darajani Sokoni na sehemu nyinginezo. Chanzo cha habari kimeipasha Global Publishers kikisema kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya familia kupoteza mali zao.

Baadhi ya wanafamilia wakiwa wamesimama barabarani baada ya nyumba zao kuzungukwa na maji.
Muonekano wa eneo la Darajani Sokoni, Bukoba

PICHA NA FAUSTINE RUTA – BUKOBA

Comments are closed.