The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Mwili wa Magufuli Utalala Ikulu Zanzibar – Video

0

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kwa kuwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo mwili wake utalala katika Ikulu ya Zanzibar usiku wa leo Machi 23, 2021 kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza kuagwa.

 

Majaliwa amesema hayo leo katika Uwanja wa Uhuru Zanzibar wakati wa zoezi la kuaga mwili wa kiongozi aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzema jijini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo.

 

“Bado tupo kwenye siku za huzuni tangu Rais wetu Suluhu Samia alipolitangazia Taifa kifo cha mpendwa wetu aliyekuwa Rais wetu, jemedari wetu ambaye ametangulia mbele za haki, pia akaelekeza tutakuwa kwenye maombolezo kwa siku 21.

 

 

“Leo mtapata fursa ya kupita mmoja mmoja mbele ya jeneza na kumuaga, tunaamini kwa idadi hii haiwezi kuchukua masaa mengi, lakini tutakuwa hapa hata kama tutamaliza saa sita usiku ili kila mmoja amalize kiu ya kumuaga kiongozi wetu.

 

 

“Kwa kuwa kiongozi wetu aliyetutangulia mbele za haki alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mwili wake utalala Ikulu hapa hapa Zanzibar na kesho asubuhi mwili utaondoka kwa ndege maalum kwenda jijini Mwanza,” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Leave A Reply