The House of Favourite Newspapers

Rais Mwinyi Aanika Mazito ya Magufuli – Video

0

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein amesema kuwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa mstari wa mbele kuimarisha maisha ya Watanzania kwa misingi ya haki na usawa bila kujali dini, kabila, rangi wala jinsia.

 

 

“Mwinyi amesema hayo leo katika Uwanja wa Uhuru Zanzibar wakati wa zoezi la kuaga mwili wa kiongozi aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzema jijini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo na kuongeza kuwa kifo hiki kimetuachia simanzi kutokana na upendo mkubwa tuliyonao kwake.

 

 

“Bado tuna huzuni kubwa ya kumpoteza Rais Magufuli, Serikali zetu mbili kwa ushirikiano tumefanya juhudi kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuonesha upendo kwa kuuaga mwili wa mpendwa wetu.

 

 

“Tumempoteza mwanamapinduzi mahiri wa karne ya sasa, alikuwa kiongozi mwenye uwezo na kipaji cha aina yake, kiongozi kama yeye ni nadra sana kupatikana.

 

 

“Marehemu Magufuli alikuwa ni kiongozi aliyejipambanua kwa uzalendo wa kweli, mtetezi wa wanyonge, mwenye kujivunia na kuuonea ufahari Utanzania na Uafrika wake,” amesema Dkt. Mwinyi.

 

Leave A Reply