The House of Favourite Newspapers

Magufuli ahahidi neema kwa wavuvi, wachimbaji wadogowadogo Mwanza na Geita

0

Magufuli akihutubia nyomi la watu lililofurika katika Kijiji cha Nkome, Geita VijijiniDk John Magufuli akihutubia nyomi la watu lililofurika katika Kijiji cha Nkome, Geita Vijijini.

magufuli leo alitembelea kijiji cha Katoma Geita vijijini na kuzuru makaburi ya babu yake Marko Nyahenga na bibi yake Anastazia (1)
Magufuli akizuru makaburi ya babu yake  Marko Nyahenga na bibi yake Anastazia yaliyopo kijiji cha Katoma, Geita Vijijini.magufuli leo alitembelea kijiji cha Katoma Geita vijijini na kuzuru makaburi ya babu yake Marko Nyahenga na bibi yake Anastazia (2)Ibada fupi ya maombi ikifanyika kuwaombea marehemu hao.

baada ya kuzuru makaburi hayo kwenye kijiji cha Katoma, Geita vijijini magufuli aliingia kwenye nyumba hii ya babu yake na kuwajulia hali ndugu zakeBaada ya kuzuru makaburi hayo kwenye Kijiji cha Katoma kilichopo Geita Vijijini,  Magufuli aliingia kwenye nyumba hii ya babu yake na kuwajulia hali ndugu zake.bibi huyu alinaswa na kamera yetu akimsikiliza magufuli kwa hisia kali wkt akiwahutubia wakazi wa Nkone, Geita VijijiniBibi huyu alinaswa na kamera yetu akimsikiliza Magufuli kwa hisia kali wakati akiwahutubia wakazi wa Nkone, Geita Vijijini.Linnah akikamua kwenye mkutano wa Nkome, Geita vijijini leoMsanii wa Bongo fleva, Linnah Sanga akikamua kwenye jukwaa la mkutano Kijiji cha Nkome, Geita vijijini leo
magufuli akiwahutubia wakazi wa kamangaMagufuli akiwahutubia wakazi wa Kamanga jimbo la Sengerema.Magufuli akiwamwaga sera kwa wakazi wa nkome Geita VijijiniMagufuli akiendelea kumwaga sera kwa wakazi wa Nkome, Geita VijijiniMagufuli akizungumza na wakazi wa Kalebezo, sengerema (1)Magufuli akizungumza na wakazi wa Kalebezo jimbo la Sengerema.magufuli alivyoomba kura kwa wakazi wa Buchosa kwenye mkutano uliofanyika Nyehunge, mkoani MwanzaMagufuli alivyoomba kura kwa wakazi wa Buchosa kwenye mkutano uliofanyika katika Mji mdogo wa Nyehunge, Sengerema, Mwanza.
malaikaMalaika akifanya yake jukwaani.Msafara wa Magufuli ukivuka kutoka mwanza kuelekea upande wa kamanga kupiga kampeniMsafara wa Magufuli ukitoka Mwanza kuelekea Sengerema kupitia Kamanga kwa kivuko cha Mv Samar.Ruby Mwanadada Rubby naye akifanya yake jukwaani.Temba na Chegge kama kawaida yao wakikamua kwenye mkutano uliofanyika Nkome, Geita Vijijini Chege na Temba nao kama kawa.vimbwanga vya Orijino komedy kwenye mkutano wa Nkome mkoa wa Geita (1) vimbwanga vya Orijino komedy kwenye mkutano wa Nkome mkoa wa Geita (2) Vimbwanga vya Ze Orijino Komedi, kijiji cha Nkome.wakazi wa Bugulula wakimuangalia magufuli wakiwa juu ya mapaaWakazi wa Bugulula wakimsikiliza Magufuli wakati wakiwa juu ya paa.wakazi wa Geita vijijini wakionesha furaha ya kumkubali magufuliuWakazi wa Geita Vijijini wakionesha furaha ya kumkubali Magufuli.wakazi wa Jimbo la Buchosa wakiinua mikono kuonesha kumkubali magufuli kwenye mkuatno uliofanyika NyehungeWakazi wa Jimbo la Buchosa wakiinua mikono kuonesha kumkubali Magufuli kwenye mkuatno uliofanyika Nyehunge.wakazi wa lwezera wakimfurahia magufuli

 Wakazi wa Lwezera wakimfurahia Magufuli.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli leo alitoka Jiji la Mwanza Mjini na kuvuka kivuko cha Kamanga kupitia Sengerema hadi Mkoa wa Geita ambapo alifanya mikutno 17 ya kampeni.
Baadhi ya mikutano aliyoifanya mkoani Mwanza katika Majimbo ya Sengerema na Buchosa ni Kamanga, Nyamatongo, Katunguru, Kasenyi, Nyamazugo, Luchiri, Bukokwa yote ya Sengerema, mengine ni Kalebezo na Nyehunge ya Jimbo la Buchosa. Pia Magufuli alifanya mikutano katika vijiji vya Lwezera, Nzera, kabla ya kuingia mkoani Geita katika Kijiji cha Katoma ilipoanzia asili yake. Akiwa Katoma magufuli alipata fursa ya kuzuru makaburi la babu yake Marko Nyahenga na bibi yake Anastazia Ntabu.
Baada ya kuzuru makaburi hayo aliendelea na kampeni katika kijiji cha Nkome kilivyopo jimbo la Geita Vijijini ambapo ulifanyika mkutano katika viwanja vya kijijini hapo, mkutano uliofurika umati mkubwa wa watu ambapo wengine walilazimika kusikiliza mkutano huo wakiwa juu ya miti ili wasikilize Magufuli.
Wasanii nao walipata fursa ya kipekee ya kutoa burudani kabla ya mkutano huo kuanza. Baada ya mkutano huo Magufuli aliendelea na kampeni zake katika vijiji vya Igate, Kasota na Bugulula vyote vya Geita Vijijini.

Katika mikutano hiyo Magufuli aliwaahidi wakazi hao kuwaboreshea miundombinu ya uvuvi katika Ziwa Victoria kwa kuwapatia wavuvi wadogo mikopo na kuwaletea vitendea kazi bora.

Akiwazungumzia wachimbaji wadogo wa madini nao aliwaahidi kuwaboreshea kazi yao.

Magufuli aliwaahidi wakazi hao kuwaongea huduma ya zahanati bora zitakazotoa huduma bila ubabaishaji na kuwaboreshea barabara za maeneo hayo kwa kiwango cha lami ili kuzipa soko biashara zitakazokuwa zikifanyika ukanda huo.

 HABARI / PICHA NA RICHARD BUKOS GPL/ ALIYEKUWA MWANZA NA GEITA
Leave A Reply