The House of Favourite Newspapers

‘Gia’ ya Rais Magufuli Ndani ya Chama Yawakosha Nguvu CCM

1Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar, Juma Simba, akizungumza na wanahabari.
2…Akisikiliza maswali ya wanahabari.
3Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimempongeza Rais John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa utendaji wake uliodhamiria kuleta mabadiliko ya kweli katika serikali na chama chake.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,  Juma Simba,  alipozungumza na wanahabari ili kumpongeza Magufuli kwa jinsi alivyoendesha vikao vya CCM vilivyomalizika majuzi kwa muda mfupi na kufanya uteuzi wa baadhi ya nafasi zilizokuwa wazi.

Amesema pia mabadiliko 23 ya chama hicho yaliyopitishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) jijini Dar ambapo idadi ya wajumbe na idadi ya vikao vilipunguzwa ni jambo lenye ishara na nia njema.

Aidha pia sekretarieti ya CCM iliyofanya vikao na mwenyekiti kuteua  nafasi zilizokuwa wazi baada ya waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ambao ni Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa na Nape Nnauye ambaye sasa ni  Waziri wa  Habari,  na Rodrick Mpogolo aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Bara akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Rajabu Luhwavi aliyeteuliwa kuwa balozi.

Mambo mengine ambayo CCM Dar inampongeza ni juhudi zake za kuhakikisha serikali inakusanya kodi kikamilifu ili kuiwezesha nchi kusonga mbele na kuahidi kuwapa ushirikiano walioteuliwa kuchukua nafasi zilizokuwa wazi.

Na Denis Mtima/GPL

Irene Uwoya Afanya Kufuru Birthday Yake, Amkumbuka Samwel Sitta Aliyezaliwa Naye Des. 29

Comments are closed.