The House of Favourite Newspapers

Balozi Wa Urusi Nchini Uturuki Auawa Kwa Risasi Akihutubia

balozi-wa-urusi-nchini-uturuki-auawa-kwa-risasi-akihutubia

ANKARA: Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrey Karlov (62) ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akihutubia jana Jumatatu usiku mjini Ankara, Uturuki.

Baada ya kumpiga risasi balozi huyo na kuanguka, muuaji huyo Mevlut Mert Aydintas mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni askari polisi wa kikosi cha kupambana na ghasia aliyekuwa zamu kwenye Mji Mkuu wa Uturuki, Ankara, alimsogelea balozi na kumpiga risasi nyingine tena kifuani.

balozi-wa-urusi-nchini-uturuki-auawa-kwa-risasi-akihutubia-2Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrey Karlov akihutubia.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amesema kuuawa kwa balozi wa taifa lake nchini Uturuki, Andrey Karlov ni uchokozi ambao lengo lake ni kuvuruga juhudi za kutafuta amani Syria huku Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, alisema kuuawa kwa balozi huyo ni shambulio dhidi ya taifa la uturuki.

Picha za video zilimuonesha mshambuliaji, akiwa amevalia suti na tai, akimfyatulia risasi balozi huyo kutoka nyuma, akisema kwa sauti ujumbe kuhusu mji wa Aleppo, Syria kwa kusema maneno haya; “Don’t forget Aleppo. Don’t forget Syria” (Usisahau Aleppo, Usisahau Syria). Imeelezwa kuwa, mshambuliaji huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

putinRais Vladimir Putin

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji hayo ambayo yametokea siku moja baada ya maandamano kufanyika Uturuki kupinga hatua ya Urusi kumuunga mkono Rais wa Syria, Bashar al-Assad.

balozi-wa-urusi-nchini-uturuki-auawa-kwa-risasi-akihutubia-1Muuaji akitamba

Recep Tayyip Erdogan alizungumza na Bw Putin kwa njia ya simu, na kwenye ujumbe wa video, alisema wote wawili wamefanya mazungumzo na kukubaliana kuwa kisa hicho kilikuwa ni cha “uchokozi”. Alisema wale waliotaka kuharibu uhusiano baina ya nchi hizo mbili hawatafanikiwa.

Bw Putin kwa upande wake alisema “bila shaka ni kisa cha uchokozi chenye lengo la kuvuruga kurejea hali ya kawaida kwa uhusiano wa kidiplomasia na shughuli ya kutafuta amani Syria”.

muuaji-wa-balozi-uturuki-1

Katibu Muu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mauaji hayo. Mawaziri wa Marekani, Uingereza, Ujerumani pia wameshutumu mauaji hayo.

Kundi linaloongozwa na kiongozi wa kidini aliyetorokea Marekani Fethullah Gulen pia limelaani mauaji hayo na kujitenga na muuaji huyo.

muuaji-wa-balozi-uturuki-2Makamada wa polisi wakiwasili eneo la tukio

Wachunguzi kutoka Urusi wametumwa Uturuki kuchunguza kisa hicho, msemaji wa Bw Putin, Dmitry Peskov amesema

Karlov, 62, ni balozi wa muda mrefu wa Urusi na alifanya kazi kama balozi wa Muungano wa Usovieti nchini Korea Kaskazini miaka ya 1980. Baada ya kuvunjika kwa muungano huo mwaka 1991, alifanya kazi kama balozi Korea Kusini kwa miaka kadha kabla ya kurejea Korea Kaskazini mwaka 2001 ambapo baada ya miaka kadhaa alitumwa Ankara mnamo Julai 2013.

 

Inasikitisha: Huyu ndiye mrembo aliyenaswa kwa ujambazi Dar

 

Comments are closed.