The House of Favourite Newspapers

Magufuli kiboko… awahenyesha Makatibu Wakuu wa Wizara

0

magufuli (2)Rais Dk. John Pombe Magufuli alipofanya Mkutano na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali.

Na Waandishi Wetu

ZIARA mbili tu alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwenye Wizara ya Fedha na kukuta wafanyakazi sita wamekwenda ‘brekfasti’ na ile ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kukuta mashine za MRI na CT Scan ziko hoi, tayari nchi imetikisika ambapo sasa kila mtumishi wa serikali analinda kibarua chake kwa kufuata masharti ya ajira.

IMG_9863Elisante Ole Gabriel.

Kufuatia ‘shtukiza’ hizo, sasa kila mkuu wa kitengo kwenye ofisi za serikali, anasimamia vyema uadilifu na wafanyakazi wake kwa kuwa ‘hawajui siku wala saa’ ambayo Magufuli ataibukia hapo.

mmbandoDonald Mmbando

Novemba 10 na 11, mwaka huu, timu ya waandishi wa gazeti hili ilidamkia kwenye wizara mbalimbali zilizopo jijini Dar kwa lengo la kujionea wafanyakazi wanavyowahi au kuchelewa katika kipindi hiki cha ‘Hapa Kazi Tu’.

Pia, Uwazi ilitaka kujua kama makatibu wakuu wa wizara hizo ambao kwa sasa ndiyo wasimamizi wakuu baada ya kutokuwepo kwa mawaziri, wanawahi maofisini au bado wanakwenda kwa ‘mwendo wa kizamani’.

meruAdelhelm Meru

Saa moja na nusu juu ya alama, Uwazi lilitia timu kwenye Wizara ya Ujenzi kwenye makao yake makuu maeneo ya Posta na kukuta katibu mkuu wake, Mhandisi Mussa Iyombe ameshafika ‘siku nyingi’. Gari la katibu huyo lilikuwa kwenye maegesho.

afyaJengo la Wizara ya Afya

Mwandishi wetu aliweza kupiga picha, lakini kabla hajatoka, alitiwa mbaroni na walinzi wa wizara hiyo baada ya simu kupigwa getini na kujulishwa kuwa, kamera za ulinzi (CCTV) zimemwona mtu akipiga picha.

Hata hivyo, baadaye walinzi hao walimwachia mwandishi huyo kwa vile hakuwa na silaha yoyote.

nishatiJengo la Wizara ya Nishati na Madini

Mwandishi mwingine, muda huohuo alivamia Wizara ya Habari, Utamaduni Vijana na Michezo iliyopo Posta ambapo katibu mkuu wake ni Profesa Elisante Ole Gabriel na kuambiwa na walinzi kuwa, bosi huyo alikwishakaa kwenye kiti chake.
maliasiJengo la Wizara ya Maliasiri na Utaliimiundombinu Jengo la Wizara ya Uchukuzi

Ili kuendelea kujiridhisha na uchunguzi wake, Uwazi liliibukia Wizara ya Uchukuzi maeneo ya Posta na kumkuta Katibu Mkuu, Shaaban Mwinjaka ameshapita langoni kuingia ofisini kwake.

Siku ya pili, Uwazi likajihimu kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii maeneo ya Keko na kuambiwa na mlinzi kuwa, Katibu Mkuu, Dk. Adelhelm Meru hajafika. Uwazi lilipiga kambi lakini katika hali ya kushtukiza, ndani ya dakika kumi aliingia na kuwahi muda wa kuingia kazini kwa watumishi wa serikali ambao ni saa 1:30 mpaka saa 2:00 asubuhi.

Uwazi lilibahatika kuzungumza na katibu mkuu huyo ofisini kwake kwa kumuuliza kuhusu maendeleo ya Hoteli ya Embassy iliyopo maeneo ya Posta ambayo mmliki wake ni wizara hiyo. Katibu mkuu huyo alikuja mbogo akimwambia mwandishi hawezi kujibu swali hilo kwani yeye anajua kila kitu.

Pia, Mwandishi mwingine wa Uwazi aliwasili kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini katibu mkuu wake, Donald Mmbando  alishafika na mlinzi aliweka ngumu kumwona kwa madai kwamba tayari alikuwa kwenye kikao cha kila siku na wafanyakazi wa wizara hiyo.

“Unajua siku hizi huwezi kukuta katibu mkuu amechelewa. Magufuli anawahenyesha ile mbaya. Sasa kama mtu hataki kazi, achelewe aone,” alisema mfanyakazi mmoja wa wizara hiyo bila kutaja jina lake.

Leave A Reply