The House of Favourite Newspapers

Uwazi latoa msaada wa viti vya wagonjwa, Moi

0

1.Ofisa uhusiano wa Global Publishers, Soud Kivea (katikati) akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).Afisa Tawala wa Global Publishers, Soud Kivea (katikati) akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
2.Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano MOI, Patrick Mvungi, Ofisa Uhusiano wa Global Publishers, Soud Kivea na Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI , Juma Almasi.Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa Moi, Patrick Mvungi, Afisa Uhusianio wa Global, Soud Kivea na Meneja Uhusiano wa Moi, Juma Almasi.
3.Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
4.Waandishi wa habari wakichukua tukio.Waandishi wa habari wakichukua habari ya tukio hilo.
5.Soud Kivea (katikati) akimkabidhi Wheel Chair Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Juma Almasi anayeshudia ni afisa uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi.…Soud Kivea (katikati) akimkabidhi viti hivyo maalum Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Juma Almasi anayeshudia ni Afisa Uhusiano wa Moi, Patrick Mvungi.
6.Baadhi ya Wheel Chair zilizotolewa kwa niaba ya Gazeti la Uwazi .Baadhi ya viti hivyo maalum vilivyotolewa na Gazeti la Uwazi .
7.Ofisa uhusiano wa Global, Soud Kivea (katikati) akiwaoneha viti hivyo jinsi vilivyo.…. Soud Kivea (katikati) akiwaonesha viti hivyo jinsi vilivyo.
8.Meneja uhusiano wa MOI, Juma Almasi akionekana kufurahia zawadi hizo.Meneja Uhusiani wa Moi, Juma Almasi akionekana kufurahia zawadi hizo.

GAZETI la Uwazi linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers, chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Eric Shigongo limetoa msaada wa viti 10 maalum vya magurudumu vya wagonjwa (Wheelchair) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi, Dar.

Akizungumza mbele ya wanahabari waliohudhuria hafla hiyo ya utoaji msaada iliyofanyika Moi leo, Afisa Tawala wa Global Publishers, Soud Kivea amesema kuwa lengo kubwa la kusaidia msaada huo ni kutambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hiyo kwa jamii hususan wagonjwa wanaohitaji huduma ya mahitaji maalum ya viti vya kutembelea na hata kwa huduma zingine za hospitalini.

Amesema Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu ni kitengo ambacho husaidia jamii kubwa ukilinganisha baadhi ya matukio yanayotokea mikoani hulazimika kuhitaji kupata huduma kutoka kitengo hicho cha Moi.

Alibainisha kuwa fedha iliyopatikana kutokana na mauzo ya Gazeti la Uwazi zimesaidia kutimiza lengo la kununua viti hivyo 10 maalum vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu.

Kivea aliongeza kuwa Gazeti la Uwazi halitasita kuendelea kutoa msaada pale patakapohitajika kwa kutambua huduma zinazotolewa ndani ya jamii hasa katika kitengo hicho kinachoshughulikia pamoja na mambo mengine, magonjwa ya mifupa.
Naye Meneja Uhusiano wa Moi, Juma Almasi amelishukuru Gazeti la Uwazi na mkurugenzi wake, Eric Shigongo kwa moyo wao wa kujitolea waliouonesha.

Amesema msaada huo utawawezesha wagonjwa wenye mahitaji maalumu kutumia viti hivyo kwenye hospitali hiyo na akasema ni jambo la kushukuru na kuigwa kwa kutambua na kuthamini wagongwa wasioweza kutembea au wenye kuhitaji huduma za haraka.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

Leave A Reply