The House of Favourite Newspapers

Mahakama Nchini Kenya Yazuia Uamuzi wa Rais Magufuli Kuepeka Madaktari 500

KENYA: Mahakama ya Kazi nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.
Jaji Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo ametoa amri hiyo baada ya Madaktari watano wa Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango wake wa kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari wengi nchini humo ambao hawajaajiriwa.
Madaktari hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari 1,400 ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na iizuie serikali kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa afya kutoka nje.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kukubali ombi lilitolewa na Rais Uhuru Kenyatta wa kuipatia Kenya madaktari katika kusaidia utoaji tiba baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo wenye lengo la kushindikiza waboreshwe maslahi yao.
Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.