The House of Favourite Newspapers

Omog Amtia Jeuri Mavugo, Aiue Kagera Sugar

STORI: Sweetbert LukongeCHAMPIONI JUMAMOSIDar es Salaam

KIKOSI cha Simba kesho Jumapili kinashuka uwanjani kupambana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Katika kuhakikisha Simba inaibuka na ushindi, Kocha wa Simba, Joseph Omog, ametoa majukumu mazito kwa washambuliaji wake hasa Laudit Mavugo ambayo wanatakiwa kuyafanya ili ushindi upatikane.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Omog alisema majukumu aliyotoa kwa washambuliaji wake hao ni kuhakikisha wanaiongoza timu hiyo kupata mabao ya kutosha katika mchezo huo lakini pia Mavugo kuhakikisha anaiendeleza rekodi yake ya kufunga mfululizo.

Omog alisema jambo jingine ni kwamba amewataka washambuliaji wake kucheza kwa ushirikiano mkubwa ili wapate mabao.

“Hayo ndiyo mambo muhimu ambayo nimewataka washambuliaji wangu kuhakikisha wanayafanya ili tuweze kuibuka na ushindi ili tuweze kujitengenezea mazingira mazuri ya kuibuka mabingwa msimu huu,” alisema Omog.

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.