The House of Favourite Newspapers

Mahakama ya Juu kuamua iwapo Trump anaweza kuwania urais

0

Mahakama ya Juu nchini Marekani imesema itasikiliza kesi ya kihistoria kubaini iwapo Donald Trump anaweza kuwania urais.

Majaji walikubali kupokea rufaa ya Bw Trump dhidi ya uamuzi wa Colorado wa kumuondoa kwenye kura ya 2024 katika jimbo hilo.

Kesi hiyo itasikizwa mwezi Februari na uamuzi huo utatumika nchi nzima.

Kesi katika majimbo kadhaa zinataka kumuondoa bwana Trump kwa madai kwamba alihusika na uasi wakati wa ghasia za Bunge la Marekani miaka mitatu iliyopita.

Changamoto za kisheria zinategemea iwapo marekebisho ya katiba ya wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe yanamfanya Bw Trump kukosa sifa ya kuwa mgombea.

Marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani yanapiga marufuku mtu yeyote ambaye “amejihusisha na uasi au uasi” kushikili wadhifa wa kitaifa, lakini mawakili wa rais huyo wa zamani wanahoji kuwa haitumiki kwa rais.

Mawakili wake wamesema: “Uamuzi wa Mahakama ya kuu ya Colorado ungewanyima haki mamilioni ya wapiga kura kinyume na katiba huko Colorado na huenda ukatumiwa kama kigezo cha kuwanyima haki mamilioni ya wapiga kura kote nchini.”

Bw Trump pia amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa maafisa wa uchaguzi huko Maine wa kumwondoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombe urais wa Marekani.

POLISI LAWAMANI TENA! WADAIWA KUMKATA MGUU OSTADH na KUCHUKUA MILIONI 7 -YULE ALIYESOTA JELA MIAKA10

Leave A Reply