The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yamkatalia Kabendera Kumzika Mama Yake – Video

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imekataa ombi la upande wa utetezi la kutaka mtuhumiwa Erick Kabendera, kwenda kumuaga mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi, aliyefariki dunia Desemba 31, 2019 , kwa sababu ana kesi ya uhujumu uchumi na hakuna ruhusa ya kukata rufaa ya uamuzi huo.

 

Awali, Wakili wa Serikali,  Wankyo Simon,  alitaka mahakama itupilie mbali ombi la Wakili wa Erick Kabendera (Jebra Kambole) kuhusu kumruhusu Kabendera kutoa heshima za mwisho kufuatia kifo cha mamaye mzazi. Wakili Wankyo amesema hoja hiyo haina mashiko.

 

“Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki msiba.

 

“Mheshimiwa hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba mahakama yako isifungwe mikono,” alisema Wakili Wankyo na mahakama ikaahirisha na kwenda kushauriana hadi saa 8:45 ilipoanza kutoa maamuzi ya maombi hayo.

 

Mahakama hiyo chini ya Hakimu Janet Mtega imetoa uamuzi na kusema kuwa haina mamlaka ya kutoa ruhusa hiyo.

 

“Uamuzi wa mahakama kutomruhusu Erick Kabendera kumuaga mama yake, tunaona umekiuka misingi ya haki za binadamu. Kwa kuwa jambo hili linatakiwa lifanyike kesho, hatuwezi kukata rufaa, tunaamini mahakama ilikuwa na uwezo wa kuamua,” amesema Wakili Jebra.

 

Leave A Reply