The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yatengua Hukumu ya Kifungo cha Sugu

WAKILI Peter Kibatala leo Oktoba Ijumaa, Oktoba 11, 2019  amesema Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetengua hukumu ya kifungo cha miezi mitano alichotumikia mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’, na katibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

 

Kibatala wakili wa Sugu na Masonga amesema kuwa walikata rufaa katika mahakama hiyo baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mbeya.

 

Amesema hukumu hiyo imesomwa leo na naibu msajili wa mahakama ikieleza kuwa mwenendo mzima wa kesi ulikuwa batili kisheria hivyo mahakama kuu imetengua hukumu, mwenendo na adhabu ya kifungo.

Comments are closed.