Kabendera Ataka Kuongea na DPP

WAKILI Jebra Kambole anayemtetea mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera katika kesi namba 75/2019, jana ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi, Augustine Rwizile kuwa wanakusudia kufanya majadiliano na ofisi ya Mwendesha mashtaka kuhusu tuhuma za uhujumu Uchumi zinazomkabili Mwandishi wa habari, Erick Kabendera.

 

Awali, wakili wa Serikali Wankyo Simon aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

 

Alisema ni kweli jambo hilo lipo katika mchakato wa kuanza majadiliano na DPP, hivyo taratibu zikikamilika wataipa taarifa mahakama. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 24 itakapotajwa tena.

Ni kongamano la JKK linafanyika katika ukumbi wa BCIC Mbezi Beach Jogoo jijini Dar es Salaam….


Loading...

Toa comment