The House of Favourite Newspapers

Messi: Mabeki Wa Uingereza Wagumu Sana

NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amekiri kuwa alijua Neymar wa PSG atajiunga na Real Madrid wakati wa dirisha la usajili lililopita baada ya kuona Barcelona watashindwa kumsajili.

 

Messi amesema hayo alipokuwa akihojiwa katika Kituo cha RAC1, ambapo alisema: “Alionyesha nia ya kuondoka Paris na nikajua Florentino (Perez) na Real Madrid watamfuata kumsajili.”

 

Mambo mengine ambayo alizungumza kwenye mahojiano hayo ni kama ifuatavyo:

NYAKATI NZURI KWAKE

“Kila mwaka nimekuwa nikipambana kuongeza ubora, nafikiri ni wakati wa (Pep) Guardiola, ndipo nilipokua sana kisoka wakati huo.”

TUKIO KUBWA NA ZURI KWAKO

“Nimepata bahati ya kukutana na matukio mengi makubwa mazuri, bado kipindi cha Guardiola nilikuwa mmoja wa wachezaji bora.”

 

WAKATI MBAYA

“Mwaka 2013 na 2014. Nilipata majeraha kwa miezi miwili au mitatu nilikuwa nje.

BAO BORA

“Lile nililofunga Rome kwa kichwa na likatupa ubingwa wa Ulaya.

 

SAFU NGUMU YA ULINZI

“Hakuna moja, tumeku-tana na wapi-nzani wengi wagumu hasa timu za England, siwezi kutaja lakini wapo wengi.

 

MPINZANI BORA ALIYEKUTANA NAYE

“Ni timu ya taifa ya Hispania tulipocheza nao mechi ya kirafiki kabla ya Kombe la Dunia 2010.

 

MECHI BORA

“Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid tuliyoshinda 2-0. Ilikuwa ya kipekee na msimu huo wa 2010/11 ilikuwa dhidi ya Madrid ya Jose Mourinho.

 

KOCHA BORA

“Guardiola. Ni bora kuliko wote, Luis Enrique naye anamfuatia kwa ukaribu.”

 

KUONDOKA BARCELONA

“Niwe mkweli, kuna wakati nilitaka kuondoka, tatizo halikuwa Barcelona bali kwingine na niliona kama sitendewi haki kwa jinsi walivyokuwa wakini-chukulia

Comments are closed.