The House of Favourite Newspapers

Davido, Wizkid: Hatuna bifu tena, hapa kazi tu!

0

davido na wiz

Lagos, Nigeria

MASTAA wa muziki wa Nigeria, ambao pia wamekuwa mahasimu kutokana na kazi zao wanazofanya kufanana na kujitwalia mashabiki kibao, Davido na Wizkid wamethibitisha kumaliza kabisa tofauti zao baada ya kupanda na kutumbuiza kwenye jukwaa moja wakati wa shoo iliyofanyika Alhamisi Desemba 3, mwaka huu jijini Lagos, Nigeria.

Uthibitisho wa kumalizika kwa tofauti zao ni kutokana na video ya shoo hiyo ya club iliyosambaa mitandaoni ikumuonesha  Davido ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuanza kuimba wimbo wake wa ‘Dami Duro’.

Wakati akielekea kumaliza kuimba wimbo huo,  ghafla Wizkid naye alitokea upande wa mashabiki kabla ya Davido kumpokea kwa kumvuta mkono kisha wote kupanda jukwaani na kuendelea kuimba pamoja nyimbo zote zilizofata bila kushuka.

Mashabiki wa wanamuziki hao kwa hapa Bongo wametoa maoni yao kuhusu uamuzi wao wa kufanya shoo pamoja kuwa, sasa ni wakati wao kukaa pamoja na kufanya kazi nzuri zaidi ili kuendeleza muziki wao, kudumisha umoja kati yao na mashabiki zao na hatimaye mafanikio zaidi katika tasnia ya muziki.

Leave A Reply