The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Afungua Maonyesho ya 12 Elimu Vyuo Vikuu

0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea baadhi ya mabanda ya washiriki vyuo vikuuu.
Akizungumza jambo baada ya kutembelea mabanda.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo  amefungua amefungua maonyesho ya 12 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) ambapo takribani taasisi za elimu ya juu 80 kutoka ndani na nje ya nchi, zimeshiriki maonyesho hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Majaliwa amezitaka taasisi hizo kuandaa mikakati ya kupunguza tatizo la ajira kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi yanayoendana na soko la ajira na fursa zilizopo.

Aidha, amesema serikali itaendelea kutenga bajeti ya kutosha kwenye sekta ya elimu ili kuongeza fursa ya wanafunzi kusoma bure, kukarabati miundombinu ya shule za serikali kongwe, kutoa vifaa vya kutosha vya kufundishia wanafunzi hasa wa masomo wa sayansi  na fedha za utafiti wa maendeleo kwa ajili ya kuimarisha ubunifu wa teknolojia.

Leave A Reply