The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Atua Chato Kwenye Kaburi la Magufuli

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amefika nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli wilayani Chato mkoani Geita kuangalia kaburi lake na kumjulia hali Mama yake Mzazi Suzana Magufuli.

Waziri Mkuu Majaliwa amefika nyumbani kwa Hayati Dkt. Magufuli akiwa safarini kuelekea mkoani Kigoma kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa Wabunge katika majimbo ya Buhigwe na Mhambwe kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo katika uwanja wa ndege wa Chato alipokelewa na mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.

Leave A Reply