The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: RITA na NIDA Haziwezi Kuunganishwa – Video

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haiwezi kuunganisha taasisi za NIDA na RITA kutokana na tofauti za majukumu yake.

 

Majaliwa amesema bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Mhe. Abubakari Damian Asenga ambaye aliishauri serikali iziunganishe taasisi hizo ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa ambavyo alisema kwa sasa vinacheleweshwa sana.

 

“NIDA inatoa kitambulisho cha Taifa ambacho kinamtambulisha Mtanzania na hakitolewi kwa mtu ambaye si raia wakati RITA inatoa cheti cha kuzaliwa kikionesha kuwa umezaliwa wapi, tarehe yako ya kuzaliwa na pia wanatoa cheti cha kifo.”

 

“Niwahakikishie kuwa Mtanzania yeyote atapata kitambulisho cha uraia, tumeongeza mitambo ya uzalishaji wa vitambulisho, tumeweka mfumo mzuri wa upelekaji vitambulisho vijijini, tumeongeza idadi ya watumishi wa NIDA.”- Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 

Leave A Reply