The House of Favourite Newspapers

(VIDEO)’Majambazi’ Sita Wauawa Katika Majibizano ya Risasi na Polisi Dar

  3

Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, DCP L. J. Mkondya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

2

DCP L. J. Mkondya akionyesha silaha walizokutwa nazo watuhumiwa hao wa ujambazi.

[embedyt] http://www.youtube.com/watch?v=UhhMfnNmG-I[/embedyt]

1

Silaha walizokutwa nazo watuhumiwa hao wa ujambazi.

WATU sita waliotuhumiwa kuwa majambazi walikufa katika majibizano ya risasi na polisi Jumatatu wiki hii mchana maeneo ya Mbezi kwa Yusuf Makondeni, jijini Dar es Salaam. Hayo yalitokea kati ya watu hao na Kikosi Maalumu cha Kupambana Ujambazi wa Kutumia Silaha cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam yaliyofanyika kwa kutumia risasi.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam DCP L. J. Mkondya alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Mkondya alisema polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kulikuwa na kikundi cha watu waliokuwa na silaha kwa ajili ya kufanya tukio la ujambazi dhidi ya mfanyabiashara aliyekuwa akitoka benki ya DTB (Diamond Trust Bank) Tawi la Nyerere Road jijini Dar es Salaam na kwamba angepita katika barabara hiyo akielekea mkoani Morogoro.

Baada ya kupata taarifa hizo polisi waliweka mtego na majambazi hao wakitumia gari aina ya Toyota Carina yenye namba za usajili T970DGZ iliyokuwa na rangi ya fedha waligundua wameingia kwenye mtego wa polisi na walianza kufyatua risasi wakitumia bastola na wenzao waliokuwa wamejaa kwenye gari yao walianza kutoka huku wakifyatua risasi hovyo dhidi ya askari.

Askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwaua majambazi hao sita na kukamata bastola mbili, moja ya kijeshi ya Kichina ikiwa na risasi moja ndani ya magazini, na nyingine aina ya Browning ikiwa imefutwa namba zake na maganda sita ya risasi yaliyokutwa katika eneo hilo la tukio.

Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hosipitali ya Taifa ya Muhimbili na upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa majambazi hao.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam mnamo siku hiyohiyo majira ya saa mbili za usiku huko maeneo ya Tegeta Masaiti Mkoa wa Kinondoni, majambazi watatu wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki moja aina ya Fekon Namba MC 370 BEY wakiwa na bunduki aina ya Shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, walitelekeza begi lililokuwa na silaha hiyo pamoja na pikipiki baada ya kufukuzwa na polisi na kuamua kukimbia kwa miguu.

Wananchi wenye hasira waliwakimbiza majambazi hao na kumuua jambazi mmoja huku wengine wakifanikiwa kutorokea kusikojulikana.

Aidha polisi wanafanya juhudi za kuwafuatilia majambazi hao ili kubaini mtandao wao alisema Mkondya.
Na Hilaly Daudi/GPL

Comments are closed.