The House of Favourite Newspapers

Majimaji Leo Ushindi Lazima

0
Wachezaji wa timu ya Maji Majimaji.

 

MAJIMAJI ya Songea mkoani Ruvuma, imesema kuwa, kutokana na wachezaji wake kuwa na afya njema, leo lazima iibuke na ushindi mbele ya wenyeji wao, Ruvu Shooting.

 

Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, leo Jumamosi inacheza na Ruvu Shooting mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Msaidizi wa Majimaji, Habib Kondo, alisema wamewaandaa vijana wao tayari kwa mchezo huo na kinachowapa matumaini ya kuibuka na ushindi ni kutokuwa na majeruhi hata mmoja.

“Tupo vizuri kupambana na Ruvu Shooting, hivyo wapinzani wetu wajipange kupokea kichapo kwani malengo yetu makubwa ni kuondoka na pointi tatu, haijalishi kama tupo ugenini.

 

“Hatuna majeruhi ndiyo maana tumekuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi kwani tutakuwa na wachezaji wote, kilichobaki ni kuchagua nani aanze ili tupate matokeo mazuri,” alisema Kondo.

 

Majimaji ipo nafasi ya nane katika ligi kuu ikiwa na pointi 11 ambapo katika mechi kumi, imeshinda michezo miwili, imetoka sare tano na kufungwa mara tano.

Stori: Martha Mboma, Championi Jumamosi

 

Leave A Reply