The House of Favourite Newspapers

Makaburi ya Vigae si Salama

 

TAARIFA za watafiti zimeeleza kuwa matumizi ya maru maru (tiles, marble, terrazzo) katika kujengengea makaburi siyo salama kwa ardhi, kwani yana kemikali kali ambayo inaathiri udongo.

 

Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa Sayansi ya Mazingira na Kilimo, Prof. Julius Zake kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, katika ripoti yake ya udongo wa Uganda huku akieelza njia sahihi ya kutumia mbolea na kueleza kwamba ujenzi wa makaburi kwa tiles unaongeza hatari kubwa ya udongo kushindwa kuzalisha.

 

“Zamani watu walikuwa wanatumia nguo maalum (backcloth ) kuzikia wapendwa wao, sasa hivi watu wanakufa sana na wanazikwa kila mahali kwa wingi,tiles haziwezi kuharibika zinaingiliana na mizizi inayorutubisha udongo na kusaidia uzalishaji, hivyo udongo unaathirika na kemikali”, amesema mwanasayansi huyo.

 

Mtaalamu huyo amesema ardhi sasa hivi imekuwa na acid nyingi na kusabaisha kushindwa kuwa na rutuba, ya kuweza kustawisha mazao na kutunza mazingira.

CREDIT: EATV

Comments are closed.