The House of Favourite Newspapers

Makala Agness: Nililipwa Mil 11 Kwenda Kufanya Mapenzi Nigeria

0

KAMA ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea mitandaoni, basi jina la Aggy Baby siyo geni kwako. Akifahamika zaidi kwa jina la Agness wa Mahari Milioni 500, alikuwa gumzo mitandaoni baada ya kutangaza kwamba mwanaume anayetaka kumuoa anapaswa kulipa mahari ya shilingi milioni 500.

 

Kama hiyo haitoshi, akazua tena gumzo kwa kumpa ofa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ya kumuoa bure kutokana na kukoshwa na uwezo wake uwanjani.

Mbali na drama za hapa na pale, Aggy Baby ambaye jina lake halisi ni Agness Suleiman amejitwalia umaarufu kupitia Tamthiliya za Panguso na Huba zinazorushwa DSTV.

 

Kubwa kabisa ni msanii mkali wa Bongo Fleva akiwa amesikika kwenye ngoma kadhaa zikiwemo Wanipa na Watajuaje zinazokiwasha kwenye miandao mbalimbali;

 

Gazeti la IJUMAA limepiga stori na Aggy Baby ambapo amefunguka mambo mbalimbali kuhusu maisha yake;

IJUMAA: Tumekuzoea kwenye uigizaji, ila sasa tunakuona pia umeingia kwenye muziki, kipi cha kwanza?

AGGY BABY: Kwa mara ya kwanza nilianza na uigizaji, niliitwa na Jimmy Mafufu kuigiza kwenye Tamthiliya ya Panguso ya DSTV. Hapo ndipo wengi walipoanza kunitambua, nikiigiza katika uhusika wa mwanadada aitwaye Vero. Baada ya hapo nimeigiza katika Tamthiliya ya Huba kama mwanasheria.

 

IJUMAA: Kwenye muziki umeingia miguu miwili au unapima upepo?

AGGY BABY: Mimi ni mwanamuziki kabisa na hii ni kwa sababu muziki unalipa zaidi ya uigizaji. Nilianza kujijua kama nina kipaji cha muziki tangu nikiwa shule ya msingi ambapo nilikuwa kiongozi wa bendi ya shule.

IJUMAA: Ni mafanikio gani uliyoyapata kwenye muziki?

 

AGGY BABY: Kama nilivyosema, muziki nimetoka nao mbali na japo bado sijapata mafanikio makubwa, tayari nauona mwanga. Tayari nimefanya ngoma na maprodyuza wa wasanii wakubwa kama LG ambaye ni prodyuza wa Zuchu na Jaga Bantu prodyuza wa P-Square.

IJUMAA: Tunaona wasanii wengi wakiachia EP na albam kwa mwaka huu, vipi upande wako?

 

AGGY BABY: Inshallah, kabla ya mwaka kuisha nitaachia EP yangu yenye takriban nyimbo 11.

IJUMAA: Nje ya muziki unafanya shughuli gani?

AGGY BABY: Ni mfanyabiashara, nina maduka ya vipodozi na nguo, Dar na Mwanza.

IJUMAA: Tunakuona ni mtoto wa mjini uliyejipatia umaarufu mitandaoni, vipi kuhusu elimu yako?

 

AGGY BABY: Ni msomi wa chuo kikuu, nina Shahada ya Usimamizi wa Fedha.

IJUMAA: Mara ya mwisho kutuma CV kuomba kazi ilikuwa lini?

AGGY BABY: Niliwahi kuajiriwa kwenye benki moja, lakini niliacha kwa sababu haikuwa kazi ambayo nilikuwa naipenda. Mara ya mwisho kutuma CV kwa ajili ya maombi ya kazi ilikuwa ni mwaka 2016.

 

IJUMAA: Kuna kipindi ulihusishwa kutoka kimapenzi na Uchebe aliyekuwa mume wa Shilole, ilikuwa ni kweli au ni kiki tu?

AGGY BABY: Ilikuwa ni kweli, lakini mapenzi yetu hayakufika mbali.

IJUMAA: Ulitangaza mahari ya shilingi milioni 500 kwa mwanaume anayetaka kukuoa, vipi alipatikana?

AGGY BABY: Wapo wanajitokeza, lakini sijaona vigezo ninavyovihitaji, pia hakuna aliyefika mahari ya shilingi milioni 500.

 

IJUMAA: Kuna faida yoyote umepata kupitia umaarufu wako?

AGGY BABY: Ndiyo, faida zipo. Mfano kupitia umaarufu wangu nimeweza kupata ubalozi wa kampuni mbalimbali japo bado hazijawa wazi. Pia nimeongeza kujiamini, naweza kusimama popote na kuongea chochote.

IJUMAA: Kila jambo lina changamoto, vipi unapitia changamoto gani kwa umaarufu wako?

 

AGGY BABY: Changamoto ni nyingi, watu wananichukulia kama dada wa mjini ambaye nafanya kazi za kudanga tu. Pia mastaa wa kike wengi wananichukia, wananiona kama natafuta kiki ili niwachukulie mabwana zao.

IJUMAA: Tukio gani kubwa ambalo hutalisahau maishani mwako?

AGGY BABY: Nakumbuka, nilitumiwa Dola za Kimarekani 5000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 11 na mwanaume mmoja ili niende Nigeria nikashiriki naye mapenzi. Sitosahau!

 

IJUMAA: Ilikuwaje?

AGGY BABY: Tulikutana mtandaoni, akaanza kunitumia ujumbe (DM) Instagram na kunieleza alivyotokea kunipenda, aliniambia anaweza akanifanya niinjoi na atanipa kila kitu nitakachohitaji.

IJUMAA: Enhe! Ikawaje?

 

AGGY BABY: Alitaka kuniaminisha kuwa anaweza kunigharamia kwa kiasi chochote cha pesa, akanitumia Dola 5,000 na kuniambia nianze kujiandaa atanitumia tiketi ya ndege ili niende Nigeria tukakutane. Sikuzikataa, nikazipokea, lakini sikwenda.

IJUMAA: Kwa nini hukwenda?

 

AGGY BABY: Sikuona haja ya kupoteza utu wangu kwa shilingi milioni 11, lakini kubwa zaidi, yule Mnigeria alinionesha dalili za kutokuwa mwaminifu tangu mwanzo kabisa kwa sababu alikuwa pia anamtaka rafiki yangu kimapenzi, nikashtuka kumbe ndiyo kazi zake, nikampiga chini.

IJUMAA: Vipi kuhusu wewe na Fei Toto, ilikuwaje umtangazie ofa ya kukuoa bila mahari?

 

AGGY BABY: Kweli nilikuwa tayari kuolewa naye bila mahari, nampenda akiwa uwanjani, yeye ndiye aliyenifanifanya nihame Simba na kuhamia Yanga, ananifurahisha!

IJUMAA: Tunaona mastaa wakila bata na mastaa wakubwa duniani, kwa mfano siku chache zilizopita tumemuona Hamisa Mobeto akila maisha na Rapa Rick Ross, upi ushauri wako?

AGGY BABY: Ninachoweza kuwaambia kuna maisha ya leo na kesho. Wasile bata wakasahau kesho!

Makala; Bakari Mahundu, Bongo

Leave A Reply