The House of Favourite Newspapers

Panga Lawapitia Watano Simba

0

SIMBA huenda ikaachana na wachezaji watano mwishoni mwa msimu huu mara baada ya mikataba yao kumalizika,
kati ya hao yupo beki Muivory
Coast, Pascal Serge Wawa.

 

Hiyo ni katika kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kitakachofanya vizuri msimu ujao kwenye mashindano mbalimbali. Tayari uongozi wa Simba umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wapyawatakaowasajili.
Mmoja wa mabosi wa Simba,
ameliambia Spoti Xtra kuwa,  wachezaji hao baadhi wataachwa kutokana na umri mkubwa walionao.


Bosi huyo alisema wachezaji
hao wamekosa kasi, hivyo Kocha Mkuu, Pablo Franco amependekeza wachezaji hao ambao majina yao yamefichwa kwa sasa.

 


Aliongeza kuwa, tayari majina
hayo kocha ameyakabidhi kwa uongozi, hivyo mwishoni mwa msimu watatangazwa.
“Zaidi ya
wachezaji watano huenda Simba wakaachana nao mwishoni mwa msimu, kati ya hao yupo Wawa.


“Kwa sasa hapati
nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, nafasi yake imechukuliwa na Inonga (Hennock) ambaye anacheza kwa kuelewana na Onyango (Joash).


“Wachezaji wengine
wanaotajwa ni wale ambao umri umekwenda na hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi
cha kwanza,” alisema bosi
huyo.


Mtendaji Mkuu wa Simba,
Barbara Gonzalez, hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema:
“Tumepanga
kufanya maamuzi magumu katika usajili wetu kwa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa watakaofanya vema katika mashindano ya kimataifa.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, Dar | CHAMPIONI

Leave A Reply