The House of Favourite Newspapers

Makamba: Hii Ndio Tanesco Mpya

0

Hii ndiyo Tanesco (Shirika la Umeme la Tanzania) mpya ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Waziri wa Nishati, January Makamba kueleza mikakati mbalimbali na mwelekeo mpya wa shirika hilo.

 

Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na uteuzi mpya wa mkurungezi wa Tanesco pamoja na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na wajumbe wake wa shirika hilo. Pia Serikali kutojihusisha moja kwa moja na uendeshaji wa Tanesco.

 

Makamba ameeleza hayo leo, Jumapili Septemba 26, 2021 katika kikao chake na watendaji wakiwemo mameneja wa wilaya, kanda na mikoa wa Tanesco pamoja na kuwatambulisha wajumbe wa bodi mpya ya wakurugenzi walioteuliwa juzi.

 

Katika kikao hicho, kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato Makamba ameeleza mwelekeo mpya wa Tanesco kwa siku zijazo. Huku akisema kumefanyika mabadiliko makubwa katika taasisi hiyo ikiwemo kuondolewa kwa watendaji mbalimbali ili mambo yaendelee.

 

“Katika mambo ya Tanesco mpya ni kwa Serikali kutojiingiza katika uendeshaji wa shirika hili. Nawaahidi kwa niaba ya Serikali hakutakuwa na uamuzi au presha za kisiasa katika uendeshaji wa shirika hili kuanzia sasa.

 

“Kuanzia sasa shirika hili la kwenu na tumewaletea uongozi mpya na bodi mpya. Imani yangu sasa tunaanza safari mpya ya uendeshaji wa Tanesco kwa namna bora yenye uweledi mkubwa,” ameongeza Makamba.

Leave A Reply