The House of Favourite Newspapers

Makamu Mwenyekiti wa Zamani Yanga Afariki Dunia

isaac-shekiondo

KLABU ya Yanga leo alfajiri imepata pigo baada ya kuondokewa na mmoja kati ya  viongozi wake wa juu waliopata kuiongoza katika miaka ya 1990, Isaac Shekiondo (pichani juu enzi za uhai wake).

Shekiondo ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa Yanga akimsaidia Abass Talimba ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu hiyo amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na tovuti hii kaka wa marehemu, Christopher Shekiondo amesema kuwa chanzo cha kifo cha Isaac aliyekuwa na miaka 58 kimetokana na matatizo ya presha na kisukari yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

“Wiki iliyopita alijisikia vibaya ndipo alipoenda hospitali moja iliyopo Kigogo, Dar kwa ajili ya matibabu lakini jana Jumamosi hali yake ilibadilika na kupelekwa Muhimbili ambapo mauti yamemfika leo.

Tovuti hii inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wote wa soka hapa nchini hususani wa Yanga kwa kuondokewa na mwanafamilia ya michezo Isaac Shekiondo.

Mwenyezi Mungu Ailaze Roho Yake Mahala Pema Peponi. AMEN.

Na  Sweetbert Lukonge

halotel-strip-1

Comments are closed.