The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Amsaidia Wheel Chair Mama Aliyegongwa na Lori

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempatia kiti cha magurudumu (wheel chair), Bi. Sidonia Ntibashigwa ambaye pia anafahamika kama Mama Sophia mkazi wa Machimbo ya Zamani, Salasala Mbuyuni, Dar es Salaam aliyepata ya ajali ya kugongwa na roli Mei 28, 2016 Mbuyuni.

 

 

Akizungumza wakati wa kumkabidhi kiti hicho Msaidizi wa Makamu wa Rais, Nehemia Mandia alisema; “Mheshimiwa Makamu wa Rais ameguswa na suala lako ambalo liliandikwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na ajali uliyoipata na ulemavu ambao umekupata kutokana na ajali. Kwa hiyo kutokana na kitendo hicho ameona akusaidie kiti cha magurudumu kwa ajili ya wewe kufanya shughuli zako ndogo ndogo unazoweza kufanya”.

Aidha, Mama Sophia alishukuru kwa msaada huo na kumuomba Makamu wa Rais aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi wake.

Alisema kwa sasa bado anaendelea na matibabu kwa kuwa mguu wake mmoja bado haujawa na nguvu hivyo hawezi kusimama. Mama huyo mwenye watoto sita na wajukuu wanne alisema pia bado anahitaji msaada ili aweze kupata matibabu zaidi.

MAMA ALIA… NATESEKA ZAIDI YA WASTARA

Kwa mara ya kwanza Bi. Sophia alifanya mahojiano na Gazeti la Amani na kuelezea matatizo anayokumbana nayo kutokana na hali yake hiyo ya afya huku akiwaomba Watanzania wamsaidie ili aweze kutibiwa. Gazeti lilikuwa chombo cha kwanza cha habari nchini kuripoti taarifa ya mama huyo.

FUMANIZI!: Mchungaji Amtoroka Mkewe Aenda kuoa “Kifaa”

Comments are closed.