The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Aongoza waombelezaji kuuaga mwili wa Hayati Edward Lowassa viwanja vya Karimjee (Picha +Video)

0

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ameongoza waombelezaji mbalimbali kutoka jijini Dar es Salam kuuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa katika shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee tarehe 13 Februari, 2024.
Viongozi wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliungana na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, vyombo vya dola, viongozi wastaafu na wananchi katika shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Hayati Lowassa.

Hayati Edward Lowassa anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Monduli, Arusha Februari 17, 2024 katika mazishi ya Kitaifa yanayotarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayati Edward Lowassa alifariki dunia tarehe 10 Februari 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Leave A Reply