The House of Favourite Newspapers

Msanii Logos Olori wa Nigeria Aachia EP Yake ya Kwanza Chini ya Davido

0

STAA wa muziki nchini Nigeria, Logos Olori ametoa albamu yake fupi (EP) akiwa chini ya lebo ya mwanamuziki nyota nchini humo, Davido.

EP hiyo inaonesha jinsi ambavyo Olori ameamua kuja kwa makali zaidi baada ya panda shuka katika gemu, mwaka uliopita wa 2023.

Katika kunogesha utamu zaidi kwenye EP hiyo, Olori amepiga kolabo na Davido katika wimbo “Easy On Me” na Musa Keys kwenye “Hmm Hmm”.

Mbali na nyimbo hizo alizowashirikisha Davido na Musa Keys, nyingine ni Olori, Push It, My Darling, Apapa na Murder zinazokamilisha nyimbo saba.

Akizungumzia project hiyo, Logos anasema: “Jiunge nami katika safari hii, tunaposafiri huku tukiwa na furaha ya ala na mitikisiko ya kila namna ya burudani. Kuanzia ngoma za Apapa hadi nyimbo tamu za Oloro, kila wimbo una tukio lake mahususi.

“Huyu ndiye Logos Olori, msanii huru, anayebadilika kulingana na kila ngoma. Ni kama maji yatiririkayo, huwa yanabadilika kila wakati yanapochukua maumbo na hali tofauti katika safari. Tuko huru na lengo ni kuwa huru siku zote.”

Bofya hapa kusikiliza EP

Leave A Reply